19 Machi 2011 - 20:30

Kutokana na mvutano mkali wa Wapalestina na Polisi wa Kizayuni waliaga Dunia Vijana 2 wa Kipalestina katika vurugu hizo, pia kusababisha mamia ya Watu kujeruhuwa katika mfutano huo.

Ripoti ya shirika la Ahlul Bayt(as)- ABNA- Katika  uvamizi wa Kizayuni Wapalestina wa 2 walifariki katika mashambulizi hayo.

Jeshi la wazayuni siku ya Ijumaa tarehe 24 February 2012 liliuwa Wapalestina wa 2 katika mvutano wa Swala Ijumaa.

Siku hiyo Wapalestina waliandamana katika sehemu mbali mbali mwa Palestina kwa kile kilofanywa na utawala haramu wa Israel.

Pia katika mvutano na vurugu hizo wanajeshi kadhaa wa Israel walijeruhiwa kwa kupigwa Mawe na wapalestina na hilo ndilo lilisababisha Waisrael kuauwa wa Palestina wa 2 kwa Risasi, pia Hospitali za Mji mkuu wa Palestina Ramallah zilieleza kuwa Mamia ya watu walijeruhiwa katika vurugu vizo.

Pia Gaza waliandamana katika kupinga mauaji hayo na kuomba Uongozi wa Gaza kuandaa maandamano kabambe ili ya kuangusha utawala haramu wa Israel.

Islah Albadoil ni mmoja wa Viongozi wa Hamas  katika maandamano ya siku ya Ijumaa alisema: mambo yanayofanywa na utawala haramu wa Israel na kuzuiya watu kuswali katika Msikiti wa Quds na kukaa kimya Ulimwengu katika swala hili ni fedheha kwa Waislamu.